ANTIFONA YA KUINGIA: Zab.33:5-6
Nchi imejaa fadhili za Bwana; kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika, aleluya!
Utukufu husemwa.
KOLEKTA
Ee Mungu mwenyezi wa milele, utuongoze hadi kushiriki furaha za mbinguni; ili sisi kundi la kondoo wako wanyonge tufike huko alikotangulia mchungaji wetu shujaa. kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo Mwanao, anayeishi na kutawala nawe katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu, milele na milele.
SOMO 1:
Mdo.13:14,43-52
Paulo na Barnaba walitoka Perge, wakapita kati ya nchi, wakafika Antiokia, mji wa Pisidia, wakaingia katika sinagogi siku ya sabato, wakaketi. Sinagogi ilipofumukana, Wayahudi na waongofu watauwa wengi wakashikamana na Paulo na Barnaba; ambao, wakisema nao, wakawatia moyo kudumu katika neema ya Mungu. Hata sabato ya pili, watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu. Bali Wayahudi walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana. Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa. Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana, Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia. Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini. Neno la Bwana likaenea katika nchi ile yote. Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watauwa wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paulo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao. Nao wakawakung'utia mavumbi ya miguu yao, wakaenda Ikonio. Na wanafunzi walijaa furaha na Roho Mtakatifu.
WIMBO WA KATIKATI: Zab.100:1-3,5 (K)3
1. Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote;
Mtumikieni Bwana kwa furaha;
Njoni mbele zake kwa kuimba.
(K)Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
au:
Aleluya!
2. Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu;
Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake;
Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake. (K)
3. Kwa kuwa Bwana ndiye mwema;
Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake vizazi na vizazi. (K)
SOMO 2:

Ufu.7:9,14-17
Wakati ule, mimi, Yohane, niliona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwanakondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao. Mmoja wa wale wazee akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwanakondoo. Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao. Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote. Kwa maana huyo Mwanakondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.
SHANGILIO: Yn.10:14
Aleluya, aleluya!
Mimi ndimi mchungaji mwema;
nao walio wangu nawajua;
Nao walio wangu wanijua mimi .
Aleluya!
INJILI:
SHANGILIO: Yn.10:14
Aleluya, aleluya!
Mimi ndimi mchungaji mwema;
nao walio wangu nawajua;
Nao walio wangu wanijua mimi .
Aleluya!
INJILI:
Yn.10:27-30
Yesu alisema, Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu. Mimi na Baba tu umoja.
Nasadiki husemwa.
MAOMBI
Ndugu wapendwa, tunasikia sauti ya Yesu anayetuita kwa njia mbalimbali. Yesu anayetuita anatuumbia moyo wa kufahamu sauti yake.
Tuombe,
1. Ee Bwana Yesu, uliahidi kutupa uzima wa kweli. Utuwezeshe kuthamini uhai wa kila mmoja kama zawadi ya thamani kubwa uliyotujalia.
2. Ee Bwana Yesu, ulisema kwamba hakuna awezaye kutupokonya katika mikono yako. Ushike mikono yetu na kutuongoza, kama ulivyoishika mikono ya Petro aliyetaka kuzama baharini.
3. Ee Bwana Yesu ulisema kwamba Baba ni mkubwa kupita vitu vyote. Utusaidie kutegemea zaidi msaada wa Mungu katika shida zetu.
4. Ee Bwana Yesu uliye mchungaji wetu: Usituache kamwe bali utuokoe katika hatari ya kujitenga nawe.
5. Ee Bwana Yesu, Uwe mwanga wetu katika giza la mashaka yetu, Uwe msaada katika shida, Uwe kimbilio katika hatari.
Ee Mungu Baba, tunakushukuru kwa njia ya Mwana wako aliyekuja kwetu awe kiongozi wetu katika mabonde ya shida na giza duniani hapa. Utusaidie tusiache kusikia sauti yake Bwana wetu anayeishi na kutawala pamoja nawe na Roho Mtakatifu, daima na milele. Amina.
SALA YA KUOMBEA DHABIHU
Ee Bwana, tunakuomba utujalie tufurahi daima katika kuadhimisha mafumbo haya ya Pasaka, ili kazi ya ukombozi inayoendelea kutimizwa ndani yetu iwe kwetu sababu ya furaha ya milele. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
ANTIFONA YA KOMUNYO: Lk.24:46-47
Amefufuka Mchungaji mwema, aliyeutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo zake, akakubali kufa kwa ajili ya kundi lake, aleluya!
SALA BAADA YA KOMUNYO
Ee Mchungaji mwema, ulitazame kwa wema kundi lako. Nao kondoo, uliowakomboa kwa damu ya thamani ya Mwanao, upende kuwaweka kwenye malisho ya milele. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.

No comments
Post a Comment