MASOMO
SOMO:1
SOMO:1
Mdo.15:1-6
Siku zile, walishuka watu waliotoka Uyahudi wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamwezi kuokoka. Basi baada ya Paulo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhojiana nao Sana, ndugu wakaamuru kwamba Paulo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemu kwa mitume na wazee kwa habari ya swali hilo. Basi, wakisafirishwa na kanisa, wakapita kati ya nchi ya Foinike na Samaria, wakitangaza habari za kuongoka kwao Mataifa; wakawafurahisha ndugu sana. Walipofika Yerusalemu wakakaribishwa na kanisa na mitume na wazee, nao wakawaeleza mambo yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao. Lakini baadhi ya madhehebu ya Mafarisayo walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika Torati ya Musa. Mitume na wazee wakakusanyika wapate kulifikiri neno hilo.
WIMBO WA KATIKATI: Zab.122:1-5
1. Nalifurahi waliponiambia
Na twende nyumbani kwa Bwana.
Miguu yetu imesimama
Ndani ya malango yako, ee Yerusalemu.
(K) Nalifurahi waliponiambia,
Na Twende nyumbani kwa Bwana.
Au:
Aleluya.
2. Ee Yerusalemu uliyejengwa
Kama mji ulioshikamana,
Huko ndiko walikopanda kabila,
Kabila za Bwana. (K)
3. Ushuhuda kwa Israeli,
Walishukuru jina la Bwana.
Maana huko viliwekwa viti vya hukumu,
Viti vya enzi vya mbari ya Daudi. (K)
SHANGILIO: Yn.10:14
Aleluya, aleluya,
Mimi ndimi mchungaji mwema,
nao walio wangu nawajua,
nao walio wangu wanijua mimi.
Aleluya.
INJILI:

Yn.15:1-8
Siku ile, Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Mimi ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. Ninyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu. Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu huyakusanya na kuyatupa motoni yakateketea. Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
MAOMBI
Ndugu, wabatizwa wote ni kama matawi ya mzabibu uliopandwa upate kuzaa matunda. Tunatambua kwamba bila Mungu ambaye ni Mzabibu wa kweli hatuwezi kufanya lolote. Katika ibada hii tumwombe: Ee Bwana Mungu:-
Kiitikio: Twakuomba utusikie.
1. Viongozi wa Kanisa wadumu katika umoja wa kitume na kutoa majibu kwa matatizo yanayowayumbisha wana Kanisa wenzao.
2. Wazee na viongozi wa nchi wasichoke kuwahimiza watu kuzishika sheria halali zenye kuleta unafuu na ubora wa maisha.
3. Sisi sote tuwe na tabia ya kuyatatua matatizo yetu ya kimwili na kiroho kwa kushirikishana mawazo na kupeana ushauri, ili tusitende kinyume cha matakwa yako.
4. Marehemu wetu wasitupwe nje ya ufalme wako, bali wasamehewe na kukusanywa pamoja na watakatifu wako huko mbinguni.
Ee Mungu, Mwanao ametuthibitishia kuwa tukiomba lolote tutakalo tutatendewa. Basi, kwa imani tunakuomba hayo tukitumaini kupata. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.

No comments
Post a Comment