MASOMO
ANTIFONA YA KUINGIA: Zab.66:16
Njoni, sikieni, ninyi nyote mnaomcha Mungu, nami nitayatangaza aliyonitendea roho yangu
KOLEKTA:
Ee Mungu mwenyezi wa milele, ulimpa wazo Bikira Maria mtakatifu, alipokuwa na mimba ya Mwanao, aende kumwamkia Elizabeti. Tunakuomba utujalie, ili, kwa kufuata mwongozo wa Roho Mtakatifu, tuweze kukutukuza daima pamoja naye. Kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo Mwanao, anayeishi na kutawala nawe katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu, milele na milele.
SOMO 1:

Sef.3:14-18
Imba, Ee binti Sayuni; piga kelele, Ee Israeli; furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, Ee binti Yerusalemu. Bwana ameziondoa hukumu zako, amtupa nje adui yako; mfalme wa Israeli, naam, yeye Bwana yu katikati yako; hutaogopa uovu tena. Katika siku ile Yerusalemu utaambiwa, usiogope, Ee Sayuni; mikono yako isilegee. Bwana, Mungu wako, yu katikati yako shujaa awezaye kuokoa; atakushangilia kwa furaha kuu, atatulia katika upendo wake. Atakufurahia kwa kuimba.
Au, la kuchagua
Rum.12:9-16
Pendo na lisiwe na unafiki; lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema. Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana; kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu; kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni, mkijitahidi. Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani. Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao. Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge.
WIMBO WA KATIKATI: Isa.12:2-6(K)6
1. Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu;
Nitatumaini wala sitaogopa;
Maana Bwana Mungu ni nguvu zangu
na wimbo wangu;
Naye amekuwa wokovu wangu.
Basi, kwa furaha mtateka maji
katika visima vya wokovu.
(K) Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.
2. Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake;
Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa,
Litajeni jina lake kuwa limetukuka. (K)
3. Mwimbieni Bwana; kwa kuwa ametenda makuu;
Na yajulikane haya katika dunia yote.
Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni;
Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako. (K)
SHANGILIO: Lk.1:45
Aleluya, aleluya!
Heri Bikira Maria aliyesadiki
ya kuwa alivyoambiwa na Bwana yatatimizwa.
Aleluya!
INJILI:

Lk.1:39-56
Mariamu aliondoka siku hizo, akaenda hata nchi ya milimani kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yuda, akaingia nyumbani kwa Zakaria akamwamkia Elisabeti. Ikawa Elisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu; akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi? Maana sauti ya kuamkia kwako ilipoingia masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu. Naye heri aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana.
Mariamu akasema,
Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,
Na roho yangu imemfurahia Mungu,
Mwokozi wangu;
Kwa kuwa ameutazama Unyonge wa mjakazi wake.
Kwa maana, tazama, tokea sasa
Vizazi vyote wataniita mbarikiwa;
Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu,
Na jina lake ni takatifu.
Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi
Kwa hao wanaomcha.
Amefanya nguvu kwa mkono wake;
Amewatawanya walio na kiburi
katika mawazo ya mioyo yao;
Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi;
Na wanyonge amewakweza.
Wenye njaa amewashibisha mema,
Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu.
Amemsaidia Israeli, mtumishi wake;
Ili kukumbuka rehema zake;
Kama alivyowaambia baba zetu,
Ibrahimu na uzao wake hata milele.
Mariamu akakaa naye kadiri ya miezi mitatu, kisha akarudi kwenda nyumbani kwake.
MAOMBI
Ndugu wapendwa, Leo tunaadhimisha sikukuu ya Bikira Maria kwenda kumtembelea Elizabeth, Ewe Mama wa Kristo, kiumbe kiteule. Tuombe.
Ee Bwana Mungu,
1. Utupe moyo wa mapendo kama Mama yetu Bikira Maria.
2. Utuepushe na dhambi za kujitenga nawe kama ulivyomkinga Bikira Maria na dhambi ya asili.
3. Kwa maombezi ya Bikira Maria aliye "Salama ya Wagonjwa." Uwasalimishe wagonjwa wa mwili na wa roho.
4. Kwa sala za Bikira Maria "Kimbilio la wakosefu." Uwahurumie wakosefu wanaokukimbilia.
5. Kwa msaada wa Bikira Maria aliye "Msaada wa WaKristo." Uwasaidie waumini wote.
6. Kwa maombezi ya Mama Maria "Malkia wa Amani." Uyajalie mataifa yote amani na raha.
7. Kwa maombezi ya Mama Maria aliye "Malkia wa Ulimwengu." Utuopoe na matetemeko ya nchi, mafuriko na majanga yote.
8. Utupokee kwako mbinguni ili tufurahi nawe na watakatifu wote.
Ee Baba wa mbinguni, twakushukuru kwa sababu mama wa Kristo ni mama yetu pia. Kwa ajili yake utulinde kwa mapendo ya kibaba, tupate kukupendeza. Kwa Kristo, Bwana wetu. Amina.
SALA YA KUOMBEA DHABIHU:
Ee Bwana mtukufu, sadaka yetu hii iletayo wokovu ikupendeze kama ulivyopendezwa na mapendo ya Mama mtakatifu wa Mwanao pekee. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
ANTIFONA YA KOMUNYO: Lk.1:48-49
Vizazi vyote wataniita mbarikiwa; kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu, na jina lake ni takatifu.
SALA BAADA YA KOMUNYO:
Ee Mungu, Kanisa lako likutukuze wewe uliyewatendea makuu waamini wako. Kanisa limtambue kwa furaha, katika sakramenti hii, yeye aliye hai daima, ambaye mtakatifu Yohane alitangulia kumtambua kwa shangwe. Anayeishi na kutawala milele na milele.

No comments
Post a Comment