SOMO:1
Mdo.7:51-8:1
Stefano aliwaambia Wakuu wa Makuhani: Enyi wenye shingo gumu, msiotahiriwa mioyo wala masikio, siku zote mnampinga Roho Mtakatifu; kama baba zenu walivyofanya, na ninyi ni vivyo hivyo. Ni yupi katika manabii ambaye baba zenu hawakumwudhi? Nao waliwaua wale waliotabiri habari za kuja kwake yule Mwenye Haki; ambaye ninyi sasa mmekuwa wasaliti wake, mkamwua; ninyi mlioipokea torati agizo la malaika msiishike. Basi waliposikia maneno haya, wakachomwa mioyo, wakamsagia meno. Lakini yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono wa kuume wa Mungu. Akasema, Tazama, naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu. Wakapiga kelele kwa sauti kuu, wakaziba masikio yao, wakamrukia kwa nia moja, wakamtoa nje ya mji, wakampiga kwa mawe. Nao mashahidi wakaweka nguo zao miguuni pa kijana mmoja aliyeitwa Sauli. Wakampiga kwa mawe Stefano, naye akiomba, akisema Bwana Yesu, pokea roho yangu. Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona vema kwa kuuawa kwake.
WIMBO WA KATIKATI: Zab.31:2-3,5,7,16,20(K)5
1. Uwe kwangu mwamba wa nguvu,
Nyumba yenye maboma ya kuniokoa.
Ndiwe genge langu na ngome yangu;
Kwa ajili ya jina lako uniongoze, unichunge.
(K) Mikononi mwako naiweka roho yangu,
ee Bwana.
2. Mikononi mwako naiweka roho yangu;
Umenikomboa, Ee Bwana, Mungu wa kweli.
Bali mimi namtumaini Bwana.
Na nishangilie, nizifurahie fadhili zako. (K)
3. Umwangaze mtumishi wako,
Kwa nuru ya uso wako;
Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.
Utawaficha katika hema
Na mashindano ya ndimi. (K)
SHANGILIO: Yn.10:14
Aleluya, aleluya,
Bwana asema: mimi ndimi mchungaji mwema;
Nao walio wangu nawajua,
nao walio wangu wanijua mimi.
Aleluya.
INJILI:

Yn.6:30-35
Siku ile, Wayahudi walimwambia Yesu: Unafanya ishara gani basi, ili tuione tukakuamini? Unatenda kazi gani? Baba zetu waliila mana jangwani, kama vile ilivyoandikwa, Aliwapa chakula cha mbinguni ili wale. Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Siye Musa aliyewapa chakula kile cha mbinguni, bali Baba yangu anawapa ninyi chakula cha kweli kitokacho mbinguni. Kwa maana chakula cha Mungu ni kile kishukacho kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima. Basi wakamwambia, Bwana, siku zote utupe chakula hiki. Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe.
MAOMBI
Wayahudi hawakumjua Yesu sawa sawa na hivi ilikuwa vigumu kwao kuamini kuwa yeye ni Mwana wa Mungu, hata wakataka ishara toka kwake. Pamoja na ishara hizo, Yeye mwenyewe aliuawa na hata baadhi ya wafuasi wake. Kwa hiyo tumwombe:
Kiitikio: Mungu wa huruma, utusikie.
1. Ee Bwana Yesu, utupe hamasa ya kuwaamini na kuwaheshimu viongozi wetu na wote wenye mamlaka katika Kanisa.
2. Wapinzani wa Neno lako wachomwe mioyo yao na kuongoka.
3. Utuepushe na tabia ya kutaka ishara za nyakati na utuongezee hamu ya kushiriki Ekaristi Takatifu.
4. Usiwahesabie dhambi zao ndugu zetu marehemu.
Ee Bwana Yesu, wewe ndiwe chakula cha uzima kilichoshuka kutoka mbinguni. Utuongezee bidii ya kuungana nawe, ili daima tuonje njaa na kiu ya kutenda yakupendezayo wewe. Unayeishi na kutawala daima na milele. Amina.

No comments
Post a Comment