SOMO:1
Mdo.9:1-20
Siku zile, Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu, akataka ampe barua za kwenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu. Hapo alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi? Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe. Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda. Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, wakiisikia sauti, wasione mtu. Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi. Basi palipokuwapo Dameski mwanafunzi jina lake Anania. Bwana akamwambia katika maono, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana. Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba; naye amemwona mtu, jina lake Anania, akiingia, na kumwekea mikono juu yake, apate kuona tena. Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemu; hata hapa ana amri itokayo kwa wakuu wa makuhani awafunge wote wakuitiao Jina lako. Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli. Maana nitamwonesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu. Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani, akamwekea mikono akisema, Ndugu, Sauli, Bwana amenituma, Yesu yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu. Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa, akala chakula, na kupata nguvu. Akawa huko siku kadha wa kadha pamoja na wanafunzi walioko Dameski. Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.
WIMBO WA KATIKATI: Zab.117(K)Mk.16:15
1. Enyi mataifa yote, msifuni Bwana,
Enyi watu wote, mhimidini.
(K) Enendeni ulimwenguni mwote,
mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
2. Maana fadhili zake kwetu sisi ni kuu,
Na uaminifu wa Bwana ni wa milele. (K)
SHANGILIO: Rum.6:9
Aleluya, aleluya,
Kristo akiisha kufufuka katika
wafu hafi tena,
wala mauti haimtawali tena.
Aleluya.
INJILI:1

Yn.6:52-59
Siku ile, Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje mtu huyu kutupa sisi mwili wake ili tuule? Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi. Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si kama mababa walivyokula, wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi milele. Maneno hayo aliyasema katika sinagogi, alipokuwa akifundisha, huko Kapernaumu.
MAOMBI
Ndugu, kwa kuongoka kwa Saulo na kwa tendo la Yesu kujifanya chakula cha roho zetu, tunakumbushwa ukweli huu kwamba hakuna lisilowezekana kwa Mungu, na kwamba tunapaswa kumtegemea Mungu daima. Kwa hiyo, tuombe:
Kiitikio: Kwa huruma yako Bwana, utusikie.
1. Uwakinge na hila za adui viongozi wetu wa Kanisa.
2. Ubariki juhudi za viongozi wa serikali na wote wenye mamlaka wanaotumia kila njia halali kupambana na maovu duniani.
3. Uwasaidie wote wanaoenda kinyume na Neno lako waongoke kwa mfano wa Mt. Paulo mtume.
4. Utuondolee woga katika utume wetu na uwashirikishe marehemu wetu maisha ya ufufuko wa Mwanao.
Kwa vile hakuna lisilowezekana kwako, Ee Mungu, utujalie udumifu katika kuyaadhimisha haya mafumbo yako matakatifu tupate kuyatangaza mauti ya Mwanao mpaka ajapo. Kwa njia ya huyo Kristo Bwana wetu. Amina.

No comments
Post a Comment