MASOMO
SOMO:1
SOMO:1
Mdo.13:13-25
Paulo na wenziwe wakang'oa nanga wakasafiri kutoka Pafo, wakafika Perge katika Pamfilia. Yohana akawaacha akarejea Yerusalemu. Lakini wao wakatoka Perge, wakapita kati ya nchi, wakafika Antiokia, mji wa Pisidia, wakaingia katika sinagogi siku ya sabato, wakaketi. Kisha, baada ya kusomwa torati na chuo cha manabii, wakuu wa sinagogi wakatuma mtu kwao, na kuwaambia, Ndugu, kama mkiwa na neno la kuwafaa watu hawa, lisemeni. Paulo akasimama, akawapungia mkono, akasema, Enyi waume wa Israeli, nanyi mnaomcha Mungu, sikilizeni. Mungu wa watu hawa Israeli aliwachagua baba zetu, akawatukuza watu hao, walipokuwa wakikaa kama wageni katika nchi ya Misri, na kwa mkono ulioinuliwa akawatoa, akawaongoza. Na kwa muda wa miaka kama arobaini akawavumilia katika jangwa. Na alipokwisha kuwaharibu mataifa saba katika nchi ya Kanaani akawapa nchi yao iwe urithi kwa muda wa miaka kama mia nne na hamsini; baada ya hayo akawapa waamuzi hata zamani za nabii Samweli. Hatimaye wakaomba kupewa mfalme; Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi, mtu wa kabila ya Benyamini, kwa muda wa miaka arobaini. Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote. Katika uzao wake mtu huyo Mungu amewaletea Israeli Mwokozi, yaani, Yesu, kama alivyoahidi; Yohana alipokuwa amekwisha kuwahubiri watu wote wa Israeli habari za ubatizo wa toba, kabla ya kuja kwake. Naye Yohana alipokuwa akimaliza mwendo wake alinena, Mwanidhani mimi kuwa nani? Mimi siye. Lakini, angalieni, anakuja mmoja nyuma yangu ambaye mimi sistahili kumlegezea viatu vya miguu yake.
WIMBO WA KATIKATI: Zab.89:1-2,20-21,26-27 (K)1
1. Fadhili za Bwana nitaziimba milele;
Kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako.
Maana nimesema, Fadhili zitajengwa milele;
Katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako.
(K) Fadhili zako, ee Bwana nitaziimba milele.
2. Nimemwona Daudi, mtumishi wangu,
Nimempaka mafuta yangu matakatifu.
Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti kwake,
Na mkono wangu utamtia nguvu. (K)
3. Yeye ataniita, Wewe baba yangu,
Mungu wangu na mwamba wa wokovu wangu.
Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza,
Kuwa juu sana kuliko wafalme wa dunia. (K)
SHANGILIO: Yn.10:27
Aleluya, aleluya,
Kondoo wangu waisikia sauti yangu,
nami nawajua, wao wanifuata.
Aleluya.
INJILI:

Yn.13:16-20
Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka. Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda. Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aliyekula chakula changu Ameniinulia kisigino chake. Tangu sasa nawaambia kabla hayajatukia, ili yatakapotukia mpate kuamini ya kuwa mimi ndiye. Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeaye mtu ye yote nimpelekaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi; ampokea yeye aliyenipeleka.
MAOMBI
Ndugu, sote tumesikia jinsi Mungu alivyowachagua baba zetu, na kuwatendea mema mengi. Hatimaye ametimiza ahadi yake ya ukombozi kwa kumtuma Mwanae aliyetangazwa na manabii. Kwa jina lake, tuombe:
Kiitikio: Pokea ombi letu.
1. Uzidi kuliinulia Kanisa lako viongozi wavumilivu na walio tayari kutumwa popote ulimwenguni. Ee Bwana.
2. Raia wote nchini wawe wakarimu kwa wasafiri, wageni na wakimbizi kadiri ya taratibu zinazokubalika na jamii. Ee Bwana.
3. Umjalie kila mmoja wetu kuutambua wajibu wa kuwapokea na kuwahudumia vema wahubiri wote wa neno lako katika jumuiya zetu. Ee Bwana.
4. Uwapokee na kuwatakatifuza marehemu wetu wote walioamini kuwa Mwanao ndiye uliyemtuma kwa ajili ya wokovu wetu. Ee Bwana.
Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.

No comments
Post a Comment