MASOMO
ANTIFONA YA KUINGIA: Zab.98:1-2
Mwimbieni Bwana wimbo mpya, kwa maana Bwana ametenda mambo ya ajabu; machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake, aleluya.
Utukufu husemwa.
KOLEKTA
Ee Mungu mwenyezi wa milele, ulitimize daima fumbo la Pasaka ndani yetu. Na hao uliopenda kuwafanya upya kwa njia ya Ubatizo mtakatifu, uwajalie wazae matunda mengi kwa msaada wa ulinzi wako, na kuzifikia furaha za uzima wa milele. Kwa njia ya Bwana wetu Yesu Krsito Mwanao, anayeishi na kutawala nawe katika umoja wa Roho Mtakatifu Mungu, milele na milele.
SOMO 1:

Mdo.14:21b-27
Paulo na Barnaba wakarejea mpaka Listra na Ikonio na Antiokia, wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi. Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila Kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini. Wakapita kati ya Pisidia wakaingia Pamfilia. Na baada ya kuhubiri lile neno katika Perge wakatelemka mpaka Atalia. Na kutoka huko wakaabiri kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwishakuitimiza. Hata walipofika wakalikutanisha Kanisa, wakawaeleza mambo yote aliyoyafanya Mungu pamoja nao, na ya kwamba amewafungulia Mataifa mlango wa imani.
WIMBO WA KATIKATI: Zab.145:8-13 (K)1
1. Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma,
Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,
Bwana ni mwema kwa watu wote,
Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote.
(K) Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza,
Nitalihimidi jina lako milele na milele.
au:
Aleluya!
2. Bwana, kazi zako zote zitakushukuru,
Na wacha Mungu wako watakuhimidi.
Wataunena utukufu wa ufalme wako,
Na kuuhadithia uweza wako. (K)
3. Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu,
Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote,
Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote. (K)
SOMO 2

: Ufu.21:1-5a
Siku ile, mimi, Yohane, niliona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kila chozi katika macho yao. Wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya.
SHANGILIO: Yn.13:34
Aleluya, aleluya!
Bwana alisema:
Amri mpya nawapa,
Mpendane, kama vile nilivyowapenda ninyi.
Aleluya!
INJILI:

Yn.13:31-33a,34-35
Yuda alipokwisha kutoka, Yesu alisema, Sasa ametukuzwa Mwana wa Adamu, naye Mungu ametukuzwa ndani yake. Mungu naye atamtukuza ndani ya nafsi yake; naye atamtukuza mara. Enyi watoto wadogo, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi. Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.
Nasadiki husemwa.
MAOMBI
Ndugu katika Kristu, kabla ya kuwaaga mitume Bwana Yesu aliwapa amri yake kuu yaani, kupendana.
Tuombe,
1. Ee Bwana Yesu, ulituachia muhtasari wa mafundisho yako yote katika amri kuu ya kupendana. Utuoneshe njia za kutimiza amri ya kupendana katika maisha yetu ya kila siku.
2. Utuhimize kuwapa wazee na wagonjwa mahitaji yote ya mwili na ya roho.
3. Utupe moyo wa kuwasaidia chakula majirani zetu ambao wamekosa chakula kwa sababu ya mavuno hafifu au matatizo mengine.
4. Utupe moyo wa kuwaona na kuwasaidia katika matatizo yao majirani zetu maskini wasiojiweza.
5. Uwape wazazi moyo wa kuwasaidia watoto wao kufikia lengo la kuwa na familia imara kwa kufunga ndoa.
6. Uwape wazazi moyo wa huruma kwa watoto wao wakorofi.
7. Uwawezeshe waumini kuwa na miradi yake ili kulitegemeza kanisa.
Ee Mungu Baba, tumeyasikia mafundisho ya Mwana wako, lakini pengine tunachelewa kuyatimiza kwa matendo. Kwa matendo ya upendo tuwavute watu wengi wajiunge na jamii ya waumini wa Yesu Kristo Bwana wetu, anayeishi na kutawala daima na milele. Amina.
SALA YA KUOMBEA DHABIHU
Ee Mungu, kwa njia ya mabadilishano matakatifu ya sadaka hii, umetufanya washirika wa umungu wako mkuu na wa pekee. Tunakuomba, utujalie ili, kama tulivyoujua ukweli wako, hali kadhalika tuweze kuufikia kwa mwenendo stahiki. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.
ANTIFONA YA KOMUNYO: Yn.15:1,5
Mimi ndimi mzabibu wa kweli, nanyi ni matawi, asema Bwana; akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana, aleluya.
SALA BAADA YA KOMUNYO
Ee Bwana, tunakuomba kwa wema wako uwe nasi taifa lako. Na sisi ulitulisha mafumbo ya mbinguni, utufanye tuondokane na maisha ya zamani, tuingie katika upya wa uzima. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.

No comments
Post a Comment